Matthew 10:26-31

26 a“Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. 27Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinong’onwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba. 28 bMsiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.
Jehanamu kwa Kiyunani ni Gehena, maana yake ni Kuzimu, yaani motoni.
29Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua. 30 dHata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. 31 eHivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

Copyright information for SwhKC